Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 18:34

Polisi Tanzania itakamata madaktari wanaogoma


Wagonjwa kwenye hospitali ya Muhimbili wamelazwa chini kutokana na ukosefu wa huduma
Wagonjwa kwenye hospitali ya Muhimbili wamelazwa chini kutokana na ukosefu wa huduma

Mgomo wa madaktari ulianza Juni 23 na madaktari wanazidi kujiunga na mgomo huo baada ya kutekwa na kupigwa kwa Dr. Steven Ulimboka

Jeshi la polisi nchini Tanzania limesema Ijumaa kuwa litaanza kuwakamata madaktari wanaoshiriki katika mgomo wa madaktari nchini humo kwa sababu wanakiuka amri ya mahakama.

Serikali ya Tanzania kupitia kwa mwanasheria mkuu wa serikali iliweka pingamizi siku moja kabla ya madaktari hao kuanza mgomo Juni 23 kuzuia mgomo huo. Lakini hata hivyo mgomo huo umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya wiki moja sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Paul Chagonja alisema jeshi la polisi lina kila sababu ya kuwakamata madaktari wanaogoma. Alisema kama madaktari hawakukubaliana na pingamizi ya serikali walikuwa na haki ya kukata rufaa sio kuendelea na mgomo.

Katika habari nyingine madaktari wanasema Dr. Steven Ulimboka ambaye alitekwa na kupigwa na watu wasiojulikana mapema wiki hii anahitaji kufanyiwa vipimo zaidi nje ya nchi.

Wakati huo huo, madaktari bingwa wa serikali za umma Ijumaa walitangaza kujiunga na mgomo kupinga kupigwa kwa Dr. Ulimboka. Jeshi la polisi limeunda tume watu watano kufanya uchunguzi wa mkasa wa Dr. Ulimboka lakini tume hiyo imepingwa na wengi ikiwa ni pamoja na madaktari wenyewe.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG