Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 16:42

Polisi Sudan walaumiwa kwa kumuuwa mwanafunzi


Polisi wakifanya doria katika mji mkuu wa Khartoum, Jumapili kusambaratisha maandamano ya wanafunzi dhidi ya serikali.
Polisi wakifanya doria katika mji mkuu wa Khartoum, Jumapili kusambaratisha maandamano ya wanafunzi dhidi ya serikali.

Wanaharakani nchini Sudan wanasema mwanafunzi mmoja ameuwawa baada ya kupigwa na polisi wakati wa maandamano ya kupinga serikali siku ya Jumapili.

Wanaharakati wanasema Mohammed Abdulrahman, mwanafunzi wa chuo kikuu cha Ahlia, alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata Jumapili jioni. Mara moja ametajwa kama “shahidi” wa kujitolea kwa ajili ya wengine kwenye ukurasa wa mtandao wa facebook, ambao awali uliitisha maandamano na sasa una kiasi cha wanachama 16,000.

Mamia ya wanafunzi walishiriki kwenye maandamano ya Jumapili katika mji mkuu Khartoum, na mji wa el-Obeid kuelekea eneo ya magharibi. Katika baadhi ya maeneo wanafunzi waliwarushia mawe polisi, ambao walijibu hali hiyo kwa kufyatua gesi ya kutoa machozi na virungu.

Polisi wa Sudan walisema wanafunzi 40 na wanafunzi 30 wengine walikamatwa. Polisi walilaani ghasia hizo.

Ahlia na chuo kikuu kimoja kingine vimefungwa Jumatatu kwa amri ya serikali. Waandishi wa habari wanasema serikali pia iliyazuia magazeti mawili binafsi ya al-Sahafa na Ajras al-Hurriya, kusambaza nakala zao.
Maandamano yalichochewa na mtandao wa Facebook uliotoa wito wa mkusanyiko wa amani dhidi ya serikali. Waandaaji walisema walitiwa moyo na maandamano ambayo yaliiondoa madarakani serikali ya Tunisia na maandamano yanayoendelea nchini Misri.

XS
SM
MD
LG