Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 04, 2024 Local time: 17:00

Polisi nchini Tanzania wapiga marufuku mkutano wa vijana wa chama cha Chadema


Mwenyekiti wa chama cha upinzani Freeman Mbowe, na wanachama wengine wakati wa mkutano wa kwanza wa chama chao baada ya kuondolewa marufuku ya kukutana, huko Mwanza, Januari 21, 2023.
Mwenyekiti wa chama cha upinzani Freeman Mbowe, na wanachama wengine wakati wa mkutano wa kwanza wa chama chao baada ya kuondolewa marufuku ya kukutana, huko Mwanza, Januari 21, 2023.

Polisi wa Tanzania Jumapili walipiga maarufuku mkutano uliokuwa umepangwa wa vijana wa chama kikuu cha upinzani, Chadema, wakiwatuhumu kupanga maandamano yenye vurugu.

Tawi la vijana wa Chadema lilikuwa limetangaza siku ya Jumamosi kwamba vijana wapatao 10,000 walitarajiwa kukutana katika mji wa kusini magharibi wa Mbeya kuadhimisha siku ya kimataifa ya vijana leo Jumatatu chini ya kauli mbiyu “chukua udhibiti wa mstakabali wako.”

Lakini Awadh Haji, mkuu wa polisi anayehusika na operesheni na mafunzo, alisema jeshi la polisi “limeona ishara za wazi kwamba lengo lao sio kuadhimisha siku ya kimataifa ya vijana bali kuanzisha na kushiriki katika vurugu.”

Taarifa yake ilitoa mfano wa vijana wa Kenya, ikionekana kumaanisha wiki kadhaa za maandamano ya kuipinga serikali katika nchi jirani ya Afrika Mashariki yaliyoongozwa kwa kiasi kikubwa na vijana.

“Polisi waliamua kupiga marufuku mkutano wa aina yoyote wa ndani na wahadhara au maandamano ambayo yamepangwa kufanyika chini ya jina la kuadhimisha siku ya vijana,” Haji alisema, akionya kuwa yanaweza kusababisha kuvurugika kwa amani.

Maafisa wa chadema wamelaani uamuzi huo, na kumtaka Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati, wakiituhumu polisi kwa kujaribu kuzuia misafara ya magari inayoelekea Mbeya na kuwakamata baadhi ya vijana.

Forum

XS
SM
MD
LG