Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 07:03

Polisi, jeshi lawasaka waliofanya shambulizi lililouwa watatu Kenya


Map of Kenya showing major cities

Maafisa wa serikali ya Kenya wanasema watu watatu wameuawa Alhamisi wakati watu wanaoshukiwa kuwa ni wapiganaji wa al-Shabab walipo lishambulia basi katika kaunti ya pwani ya Lamu.

Safari kupitia barabara ya Lamu-Garsen zimesitishwa wakati jeshi na vyombo vya usalama vikifuatilia shambulizi hilo katika eneo, katika kuwatafuta washukiwa wa uhalifu huo.

Watu watatu wengine waliokuwa ndani ya basi wameripotiwa kujeruhiwa katika shambulizi hilo. Basi hilo lililokuwa linasafiri kutoka Mombasa kwenda mji wa Lamu.

Kamishna wa Kaunti ya Lamu Irungu Macharia amethibitisha kwa vyombo vya habari kutokea kwa shambulizi hilo.

Kikundi cha al-Shabab cha Somalia kimeendelea kufanya mashambulizi mbalimbali nchini Kenya katika muongo uliopita. Kikundi hicho kinasema kinalipiza kisasi kwa kitendo cha Kenya kuchangia vikosi vyake katika Jeshi la kulinda Amani la Umoja wa Afrika AMISOM nchini Somalia.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Kenya.

XS
SM
MD
LG