Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 17, 2025 Local time: 18:50

Polisi Jacksonville yasema muuaji alikuwa na nia ya ubaguzi wa rangi na aliwachukia watu Weusi


Mkuu wa Polisi wa Jacksonville, Florida, TK Waters akizungumza wakati wa mkutano na wanahabari kuhusu mtu mwenye bunduki huko Jacksonville, Florida, Agosti 26, 2023.
.
Mkuu wa Polisi wa Jacksonville, Florida, TK Waters akizungumza wakati wa mkutano na wanahabari kuhusu mtu mwenye bunduki huko Jacksonville, Florida, Agosti 26, 2023. .

Waters anasema hakuna ushahidi kwamba mpiga risasi alikuwa sehemu ya kikundi chochote.

Mkuu wa Polisi wa Jacksonville anasema mtu mmoja mwenye bunduki mzungu ambaye aliwaua watu watatu kwenye duka liitwalo Dollar General siku ya Jumamosi, alikuwa na nia ya ubaguzi wa rangi na aliwachukia watu Weusi.

Mkuu huyo T.K.Waters anasema mshambuliaji huyo baadaye alijiua. Wanaume wawili na mwanamke mmoja waliouawa walikuwa Weusi. Waters anasema hakuna ushahidi kwamba mpiga risasi alikuwa sehemu ya kikundi chochote.

Wakazi wa Jacksonville ambao siku hiyo walihudhuria siku ya ukumbusho wa miaka 60 ya Maandamano mjini Washington na hotuba maarufu ya I Have A Dream ya Mchungaji Martin Luther King Jr. walitafakari juu ya kuendelea kwa vurugu za ubaguzi wa rangi huko Florida.

Forum

XS
SM
MD
LG