“Yanapotokea matukio ya aina hiyo ya kukamatwa au kusumbuliwa tujulishane kwa sababu baadhi ya askari wakati mwingine hufanya vitu ambavyo siyo msimamo wetu sisi viongozi wao,” alisema Mkuu wa Polisi (IGP) Ernest Mangu.
Hivi karibuni huko mkoani Arusha polisi waliwakamata waandishi ambao walikuwa wamealikwa katika shughuli ya kukabidhi michango kwa wafiwa wa wahanga wa ajali ya wanafunzi iliyotokea Karatu, mkoani Arusha.
IGP amesema waandishi na vyombo vya habari ni wadau muhimu wa jeshi hilo lazima washirikiane nao.
Vyanzo vya habari pia vimesema kuwa Mangu pia alizungumzia matukio ya mauaji yanayoendelea wilayani Kibiti Mkoa wa Pwani akisema ni uhalifu kama ulivyo mwingine wa kawaida na usitafsiriwe vinginevyo kwa sababutayari umeanza kudhibitiwa.
Aliongea hayo baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa nchi za Kusini mwa Afrika (Sarpcco) unaoendelea Arusha.
Wakati huo huo vyombo vya usalama vinawashikilia watu zaidi ya 60 katika mahabusu ya gereza la Kisongo, Arusha kwa tuhuma za kuhusika na ugaidi ikiwamo kurusha bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Olasiti.
Naye Katibu Mtendaji wa Sadc, Dr Stegomena Tax, aliwahakikishia wakuu hao wa polisi kuwa Jumuiya anayoingoza itaendelea kutoa misaada na ushirikiano kila unapohitajikakuimarisha usalama katika eneo hilo.
Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Masauni amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi wanachama wa Sadckuhakikisha uhalifu wa kuvuka mipaka unadhibitiwa.
IGP Mangu alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa