Polisi wa Fredericton wamewataka wakazi wa eneo hilo kukaa majumbani kwao, na mpaka sasa mazingira yaliyopelekea shambulizi hili hayaeleweki.
Polisi walikuwa pia wanawataka watu walioko kwenye Facebook kutotaja maeneo ambayo polisi wako kupitia mitandao ya kijamii.
David MacCoubrey, ambaye anaishi mjini Fredericton, amesema alisikia milio ya risasi 20, na anaendelea kujificha jikoni nyumbani kwake.
“Nimelala chini,” ameeleza katika mahojiano ya simu. “Askari wamekuja katika eneo langu. Wamepekuwa nyumba zote katika jengo letu. Inaelekea kama shambulizi hili lilianza katika eneo la jengo letu.”
Akiwa nyumbani kwake katika barabara ya Brookside Drive aliamka majira ya saa moja asubuhi saa za Canada, baada ya kusikia mlio wa risasi tatu futi 33 kutoka kitandani kwake.
MacCoubrey amesema eneo la jengo ambalo lina makazi yake yako majengo mengine manne yaliyoko katika eneo la mraba, na ilielekea kama sauti za risasi zilikuwa zinatoka katika jengo lilioko katikati ya eneo hilo.
Amesema polisi wamekuwa wakipekuwa majengo hayo, na yeye amekaa mbali na dirisha. “Hili sio jambo ambalo linatokea mara nyingi,” amesema.