Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 02:51

Polisi 6 wamefariki katika maandamano ya kulalamikia uchumi mbaya Sierra Leone


waandamanaji wakikimbia maafisa wa usalama mjini, Sierra Leone, Aug 10, 2022
waandamanaji wakikimbia maafisa wa usalama mjini, Sierra Leone, Aug 10, 2022

Maafisa sita wa polisi wameuwa katika maandamano ya kuipinga serikali kaskazini na magharibi mwa Sierra Leone, jumatano.

Mkuu wa polisi William Fayia Sellu, amesema kwamba maafisa wawili wa polisi waliuawa katika mji mkuu Freetown, watatu katika mji wa Kamakwie kaskazini mwa nchi hiyo na mmoja katika mji wa Makeni ulio kaskazini.

Maandamano makubwa yametokea kaskazini na magharibi mwa nchi ambapo wanasiasa wa upinzani wana ufuasi mkubwa katika nchi hiyo ya Afrika magharibi.

Raia wawili wamethibitsihwa kuuawa katika mji wa pwani wa Freetown.

Waandamanaji wanalalamikia hali ngumu ya uchumi nchini humo. Serikal imezima huduma ya internet na kuatangaza amri ya watu kutotoka nyumbani kwako kuanzia saa tisa alasiri, katika jaribio la kuzuia ghasia.

XS
SM
MD
LG