Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 20:36

Visa vipya vya polio vyagunduliwa Nigeria

Profesa Adewole, alisema visa hivyo vipya vinavunja moyo, lakini akalihakikishia taifa kwamba wizara yake itafanya chochote kiwezekanacho, kudhibiti hali hiyo.
Profesa Adewole, alisema visa hivyo vipya vinavunja moyo, lakini akalihakikishia taifa kwamba wizara yake itafanya chochote kiwezekanacho, kudhibiti hali hiyo.

Vyombo vya habari vya Nigeria vimeripoti visa viwili vipya vya polio, ikiwa ni wakati ambapo taifa hilo lingeadhimisha mwaka wa pili tangu kutangazwa taifa lililoangamiza ugonjwa huo.

Gazeti la Leadership la Nigeria, siku ya Alhamisi lilimnukuu waziri wa Afya, Profesa Isaac Adewole akisema kuwa timu ya wataalam wa chanjo ya watoto wanatumwa kwa jimbo la Borno, ambako maambukizi yameripotiwa.

Profesa Adewole, alisema visa hivyo vipya vinavunja moyo, lakini akalihakikishia taifa kwamba wizara yake itafanya chochote kiwezekanacho, kudhibiti hali hiyo.

Mwezi uliyopita kundi la madaktari bila ya miapka lilitoa taarifa mwezi uliyopita inayoeleza kwamba hali ya afya katika jimbo la Borno ni ya hatariambako zaidi ya watu elfu 50 wanahitaji kwa dharura maji chakula huduma ya afya na makazi.

XS
SM
MD
LG