Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 20:32

Serikali yajitetea kwa matumizi ya nguvu Arusha


Mkutano wa chama cha upinzani cha Chadema kumaliza kampeni za uchaguzi wa 2010 Dar es Salaam
Mkutano wa chama cha upinzani cha Chadema kumaliza kampeni za uchaguzi wa 2010 Dar es Salaam

Jeshi la Polisi nchini Tanzania limetoa tena ufafanuzi kuhusu mauaji ya raia watatu yaliyotokea huko Arusha kufuatia vurugu za kisiasa, ambapo pia watu kadhaa walijeruhiwa na viongozi wa chama cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA walifunguliwa mashtaka.

Akitoa taarifa mbele ya waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam, siku ya Alhamisi, mkuu wa oparesheni wa jeshi la polisi kamishna Paul Chagonja, amesema walilazimika kutumia nguvu za ziada baada ya juhudi zote za kuwazuia vijana waliokuwa na jazba waliochochewa na viongozi wa CHADEMA, kuvamia kituo kikuu cha polisi mkoani Arusha kushindikana.

Hata hivyo jeshi la polisi limesema bado linafanya tathmini ya athari hizo na taarifa kamili itatolewa na serikali.Kamishna Chagonja anasema, “kinachoendelea sasa huko Arusha mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai bwana Robert akishirikiana na timu ya wadau wengine wa usalama kama vile haki jinai, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na mwanasheria mkuu wa serikali bado wanaendelea na uchunguzi. Kwa lengo la kuona matukio yote yaliyotendeka makosa ya kiutendaji na kijinai kwa upande wa polisi na kwa upande wa CHADEMA, na mara atakapomaliza upelelezi wake na kundi lake hilo taarifa kamili mtaweza kupatiwa nini kilichojiri nani abebe msalaba wake.”

Katika hatua nyingine jeshi la polisi limeonya kuwa halitakubali mamlaka za nchi kuchezewa na watu wachache kwa maslahi ya kisiasa na kuonya viongozi wa vyama vya siasa kutafuta njia zinazofaa kutatua migogoro ya kisiasa.

Maelfu ya wakazi na wafuasi wa chama cha CHADEMA mkoani Arusha walijitokeza kwenye maandamano ya amani na hatimaye kuaga miili ya watu waliopoteza maisha wakati wa ghasia za kisiasa, huku viongozi wa chama hicho wakisisitiza kwamba wahusika wakuu wa maafa hayo wakiwemo viongozi wa serikali na jeshi la polisi nchini wanapaswa kujiuzulu kwa kusababisha mauaji hayo.

XS
SM
MD
LG