Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 13:24

Maafisa 3 wa polisi wauawa, 3 wajeruhiwa Louisiana

Maafisa watatu wa polisi waliuawa na wengine kujeruhiwa siku ya Jumapili baada ya mtu aliyekuwa na bunduki kuwashambulia katika mji wa Baton Rouge, Luisiana, nchini Marekani.

Na BMJ Muriithi

Maafisa watatu wa polisi waliuawa na wengine kujeruhiwa siku ya Jumapili baada ya mtu aliyekuwa na bunduki kuwashambulia katika mji wa Baton Rouge, Luisiana, nchini Marekani.

Kwa mujibu wa mamlaka za Louisiana, afisa wa nne alikuwa katika hali mahututi kwenye hospitali moja mjini Baton Rogue.

Ripoti ambazo hazikuwa zimedhibitishwa zilisema kuwa mshukiwa mmoja huenda aliuawa kufuatia makabiliano na polisi.

Vyombo vya habari viliripoti Jumapili asubuhi kuwa takriban maafisa saba walikuwa wamepigwa risasi na baadhi yao kukimbizwa hospitalini.

Shambulizi hilo lilitolkea mwendo wa saa tatu asubuhi, saa za Marekani ya kati.

Meya wa mji wa Baton Rouge Mashariki, Kip Holden, alinukuliwa na shirika la habari la CNN akisema kuwa huenda mshukiwa ni mmoja ya waliuawa lakini hakudhibitisha ripoti hizo.

Hata hivyo, alisema kuwa hali ilikuwa imedhibitiwa kufikia saa sita mchana saa za Marekani ya kati.

Tangu Mmarekani mweusi Alton Sterling kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi katika mji huo mapema mwezi Julai, hali ya taharuki imekuwa ikitanda huku mamlaka zikielezea hofu kuwa huenda kukatokea mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Kifo cha Sterling kinaaminnika kuchangia pakubwa maandamano ambayo yameendelea kushuhudiwa katika miji kadhaa Marekani, yakipinga kile wahusika wamekuwa wakikiita 'mauaji ya kijholela na polisi wanaowalenga Wamarekani weusi.'

Shambulizi hilo la Jumapili lilijiri siku tisa baada ya shambulizi lingine mjini Dallas, Texas, lililowaua maafisa 5 wa polisi na kuwajeruhi wengine kadhaa.

Taarifa zaid hivi punde...

XS
SM
MD
LG