Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 23:59

Wakurdi wadai kuhusika na mashambulizi ya Uturuki


Wanamgambo wa chama cha Kurdistan Workers Party (PKK) wamedai kuhusika na shambulizi katika kituo cha polisi Jumatano kwenye eneo la kusini mwa jimbo la Mardin na kuuwa watu sita katika eneo hilo.

“Tukio hilo kubwa lilitekelezwa katika maeneo ya kituo kikuu cha polisi katika jimbo la kifashisti katika mji wa Midyat wa jimbo la Mardin na wenzetu,” kikundi cha PKK kilieleza katika taarifa yake iliyowekwa kwenye mtandao wake.

Shambulizi hilo katika mji wa Kikurdi wa Midyat lilijeruhi watu 30.

Kikundi hicho cha PKK kimekuwa kikiwalenga polisi wa Uturuki na wanajeshi katika mapambano yake ya kutafuta uhuru upande wa kusini mashariki wa Uturuki tangu kuvunjika kwa sitisho la mapigano mwaka mmoja uliopita.

XS
SM
MD
LG