Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 27, 2022 Local time: 22:59

Philadelphia Eagles yaibuka mshindi wa Superbowl Marekani


Nick Foles (9) kapteni wa Philadelphia Eagles akimbeba binti yake, Lily James, baada ya ushindi wa NFL Super Bowl 52 Feb. 4, 2018, mjini Minneapolis.

Fainali za mpira wa Football ya Marekani maarufu kama Superbowl ikiwa ni ya 52, uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na mashabiki kati ya timu ya New England Patriots na Philadelphia Eagles umemalizika.

Mchezo huo ulikuwa unafanyika katika jiji la Minneapolis kwenye jimbo la Minnesota na timu ya Philadelphia Eagles imeibuka mshindi kwa point 41 dhidi ya 33 za New England Patriots.

Mchezaji wa Eagles, Nate Gerry akisheherekea ushindi
Mchezaji wa Eagles, Nate Gerry akisheherekea ushindi

Huu ni ushindi wa kwanza kabisa wa Eagles baada ya kufika finali mara tatu katika kipindi cha miaka 39 iliyopita. Mara ya mwisho kwa Eagles kufika finali ilikua 2005 walipokutana na hao hao Patriots walipolazwa pointi 24 kwa 21.

Katika finali ya mwaka 1981 wakati wa Superbowl ya 15 walilazwa na The Oakland Raiders kwa point 27 dhidi ya 10.

Mara baada ya kumalizika kwa mchuano huo ulotizimwa kote nchini wakazi wa Philadelphia walishuka majiani kusherekea ushindi huo wa kipekee ambao hawakutegemea kamwe.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG