Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 23:01

Peter Kenneth kuwania ugavana wa Nairobi kama mgombea huru


Peter Kenneth alitangaz tarehe 19 mwezi Mei, 2017 kwamba atawania ugavana kama mgombea huru
Peter Kenneth alitangaz tarehe 19 mwezi Mei, 2017 kwamba atawania ugavana kama mgombea huru

Aliyekuwa mgombea wa urais nchini Kenya, Peter Kenneth, alitangaza Ijumaa kwamba atawania kiti cha gavana wa kaunti ya Nairobi kama mgombea huru kwenye uchaguzi wa urais wa tarehe nane mwezi Agosti mwaka huu.

Kenneth, mwenye umri wa miaka 52, alishindwa na seneta wa Nairobi, Mike Mbuvi Sonko, kwenye uchaguzi wa mchujo uliofanyika mwishoni mwa mwezi Aprili, kutafuta tikiti ya chama kinachotawala cha Jubilee.

Kenneth alitangaza azma yake alipowahutubia waandishi wa habari mjini Nairobi.

Baada ya uchaguzi huo wa mchujo, Kenneth alilalamikia jinsi ulivyofanyika na kusema kuwa uligubikwa na dosari.

"Sitaki kujihusisha na uchaguzi huo wa Jubilee uliogubikwa na dosari chungu nzima," alisema mwanasiasa huyo mnamo tarehe 27 mwezi Aprili baada ya Sonko kutangazwa mshindi.

Kenneth, ambaye kwa wakati mmoja alikuwa mbunge aliyewakilisha eneo la Gatanga, kaunti ya Murang'a, aliwania urais mwaka wa 2013 lakini akashindwa.

Sasa anatarajiwa kushindana na Mike Sonko, gavana wa sasa wa Nairobi ambaye atawania kiti hicho kwa tikiti ya ODM, Evans Kidero, na mwansiasa mwingine anayesimama kama mgomea huru, Miguna Miguna.

XS
SM
MD
LG