Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 22:37

Rais wa Peru atoa amri baada ya basi kuua 51


Ndege yaonekana katika eneo la ajali ya basi iliyoua watu 51 nchini Peru.
Ndege yaonekana katika eneo la ajali ya basi iliyoua watu 51 nchini Peru.

Waokoaji walifanya kazi kwa saa ishirini na nne mfululizo kuiondoa miili ya watu waliokufa kufuatia ajali ya basi iliyotokea nchini Peru juzi Jumanne.

Watu 51 walikufa pale basi lilipoanguka takriban mita 100 kutoka eneo lililoinuka hadi kwenye ufuo wa bahari moja nchini Peru.

Mamlaka za Peru zimeitaja ajali hiyo kuwa mbaya Zaidi katika historia ya nchi hiyo.

Basi hilo liligongana na trela katika sehemu iliyo na barabara nyembamba iitwayo 'Devil’s curve' mjini Pasmayo, ulio Kaskazini mwa mji mkuu wa Peru, Lima.

Barabara hiyo inajulikana kama moja ya zilizo hatari mno nchini humo.

Rais wa Peru Pablo Kuczynski alitangaza Jumatano kwamba alikuwa ameiamuru wizara ya uchukuzi kupanua barabara hiyo, ili mabasi yaache kupitia sehemu hiyo hatari.

XS
SM
MD
LG