Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 15:29

Pepe Ndombe afariki kutokana na mshtuko wa moyo


Pepe NdomeOpetum,
Pepe NdomeOpetum,

Pepe Ndombe Opetum alipata umarufu wake miaka ya sabini wakati alipokua na bendi ya Tout Puissant Ok Jazz.

Ndombe Opetum maarufu YA PEPE alianza muziki akiwa na umri wa miaka 18, alianzia kwenye bendi ya Afrikan Fiesta ya Pascal Rochereau Tabu ley.

Ndombe Opetum alijipatia umaarufu baada ya kuondoka kwenye bendi hiyo ya African Fiesta kwa wanamuziki Sam Mangwana, Mavutico na wengine .

Pepe Ndombe ameacha kibao kipya cha muziki ambacho ametoka kurikodi.Mwanamuzi Adolphe Do Minguez ambae nilimkuta kwenye studio ya kurikodi nyimbo amelezea ujasiri wa Pepe Ndombe

Wizara ya utamaduni na sanaa imepanga kumuandalia maziko ya heshima mwanamuziki huyo ambae mwanae Baby Ndombe amefuata nyoyo za babake nakuwa mwanamuziki chipukizi hapa nchini.

Pepe Ndombe ametarajiwa kuzikwa wiki ijayo

XS
SM
MD
LG