Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 21, 2025 Local time: 10:45

Pendekezo la lisisto la mapigano ya Gaza latiliwa mashaka


Moshi ukipaa angani baada ya shambulizi la anga la Israel kwenye nyumba ya makazi katika mji wa Bureji, Ukanda wa Gaza. Juni 3, 20224.
Moshi ukipaa angani baada ya shambulizi la anga la Israel kwenye nyumba ya makazi katika mji wa Bureji, Ukanda wa Gaza. Juni 3, 20224.

Hatma ya pendekezo la kusitisha mapigano kwa muda huko Gaza, kuongeza misaada ya kibinadamu, na kuachiliwa kwa baadhi ya mateka wanaoshikiliwa na Hamas  kufikia Jumanne bado halina uhakika, kwa kuwa Hamas bado haijatoa majibu yake.

Maafisa wa Israel wanahoji baadhi ya maelezo, wakati Marekani ikitafuta uungaji mkono wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, katika kukubalika na kutekelezwa kwa makubaliano hayo. Pendekezo la Marekani ambalo VOA imeliona linaitaka Hamas kukubali na kutekeleza sitisho la mapigano bila kuchelewa na bila ya masharti.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Mathew Miller Jumatatu aliwaambia wanahabari kwamba Hamas ambayo ilipokea pendekezo la kusitisha mapigano Alhamisi wiki iliyopita, bado haijatoa majibu yake. Alisema kuwa sehemu kubwa ya mapendekezo hayo inaendana na pendekezo la Hamas lililotolewa wiki kadhaa zilizopita.

Baadhi ya mapendekezo kwenye mkataba wa sasa ni pamoja na wiki 6 za siltisho la mapigano, kuachiliwa kwa baadhi ya mateka waliopo Gaza, upelekaji wa malori 600 ya misaada kila siku kwa wapalestina, pamoja na kuendelea kwa mashauriano yanayolenga sitisho la kudumu kumaliza mzozo.

Forum

XS
SM
MD
LG