Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 10:30

Pence awaepuka maafisa wa Korea Kaskazini katika Olympic


Makamu wa Rais Mike Pence, kiongozi wa Korea Kusini na mwakilishi wa Korea Kaskazini walijikuta wako pamoja katika jukwaa la wageni rasmi Ijumaa wakati wa ufunguzi wa Michezo ya Olympic 2018 nchini Korea Kusini.

Hata hivyo vyanzo vya habari vimeripoti kuwa Pence alijiepusha kabisa kufanya maongezi au mawasiliano yoyote na maafisa wa Korea Kaskazini.

Pence na mkewe, Karen wakiwa wamekaa karibu na Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in, pia katika mstari mmoja na Moon aliketi Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe.

Wote wawili walikuwa wamevaa majaketi ya timu ya Marekani inayowakilisha michezo hiyo ya msimu wa baridi, yenye rangi tatu, nyekundu, nyeupe na bluu

Wakati huo huo wawakilishi wa Korea Kaskazini- Kim Yong- Nam na Kim Yo-jong- walikuwa katika jukwaa hilo wakiwa wameketi nyuma yake Pence.

Kim Yo Jong ni dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na ni mshauri mkuu wa kaka yake. Yeye ni wa kwanza katika uongozi uliopo madarakani wa Korea kwa miaka mingi kutembelea Korea Kusini tangu vita vya Korea 1950-53 kumalizika.

Kwa mujibu wa ofisi ya Pence, hapakuwa na “maongezi” kati ya makamu wa rais wa Marekani na maafisa wa Korea Kaskazini.

XS
SM
MD
LG