Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 25, 2024 Local time: 11:02

Makamu wa Rais Ametumia 'Email' Binafsi Alipokuwa Gavana


Makamu wa Rais Mike Pence
Makamu wa Rais Mike Pence

Makamu wa Rais Mike Pence amekuwa akitumia akaunti yake binafsi ya barua pepe (email) kufanya shughuli za umma wakati akiwa gavana wa Indiana, kwa mujibu wa rikodi za umma zilizochapishwa na gazeti la Indianapolis Star.

Gazeti hilo limeelezea Alhamisi kuwa barua pepe zilizotolewa kupitia maombi ya kupata rikodi hizo zinaonyesha kuwa Pence alikuwa anawasiliana na washauri wake kupitia akaunti yake ya internet (AOL), kwa shughuli za wizara ya usalama na upelelezi, akiwa nyumbani kwake, alipokuwa anatumikia nafasi ya ugavana kwa miaka minne.

Gavana huyu aliwahi kukabiliwa na masuala ya usalama katika barua pepe zake. Akaunti ya email ya Pence ilikuwa imeandamwa na aina fulani ya udukuzi mwaka jana, kabla hajachaguliwa na Donald Trump kujiunga naye katika kinyang’anyiro cha urais kwa tiketi ya Republikan.

Kulikuwa na udukuzi uliofanyika kupitia barua pepe iliotumwa ikidai kuwa gavana na mkewe walikuwa wameharibikiwa katika safari yao huko ufilipino na wanahitaji msaada wa pesa.

Lakini gavana huyo alihamia katika akaunti mpya ya internet iliyokuwa ni salama zaidi, msemaji wa Pence, Marc Lotter amesema, akiongeza kuwa aliacha kutumia akaunti yake binafsi tangu kuapishwa kwake kuwa rais.

Lotter amesema kuwa Pence “ameendelea kutumia akaunti ya email ya serikali na email yake binafsi” kama magavana waliopita katika jimbo hilo.

Wakati wakumaliza muda wake Pence aliamleta wakili kupitia mawasiliano yake yote ili kuhakikisha kuwa barua pepe zinazo husiana na shughuli za serikali zinahamishwa na kuhifadhiwa katika kumbukumbu za serikali, msemaji huyo amesema.

Wakati akiwa mgombea mwenza wa Trump, Pence mara nyingi alimkosoa Hillary Clinton kwa kutumia chombo cha kuhifadhi email- “server” wakati akiwa waziri wa mambo ya nje katika utawala wa Rais Barack Obama, akimshutumu kwa kufanya makusudi kuzificha barua pepe zake zisifikiwe na vyombo vya umma ili kujihami asichunguzwe.

Lotter amesema “kulinganisha hayo ni upuuzi” kwani Clinton alikuwa ameweka “server” nyumbani kwake wakati akianza kipindi chake katika Wizara ya Mambo ya Nje. Hii ni kinyume kabisa na Pence kwani hakuwa anashughulikia nyaraka za siri katika nafasi yake ya ugavana.

Gazeti hilo limeripoti kuwa ofisi ya mrithi wa Pence, Gavana wa Indiana Eric Holcomb, alitoa zaidi ya kurasa 30 kutoka akaunti ya Pence, na alikataa kuweka hadharani idadi isiyojulikana ya barua pepe kwa kuwa zilikuwa zinajulikana ni za siri.

Wafanyakazi wa umma hawakatazwi kutumia akaunti za email zao binafsi chini ya sheria ya Indiana, lakini sheria hiyo inatafsiriwa kuwa shughuli yoyote ya kiserikali inayofanyika kwa kutumia barua pepe binafsi ni lazima ihifadhiwe kulingana na sheria ya kumbukumbu za umma.

XS
SM
MD
LG