Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 02:15

Pato hafifu kwa kampuni za mawasiliano Kenya


Makampuni makubwa ya mawasiliano nchini Kenya yamerekodi mapato hafifu katika soko la hisa la nchi hiyo, hayo ni kulingana na mamlaka inayosimamia mawasiliano nchini humo, Communication Authority-CA.

Kwenye ripoti ya robo ya kwanza ya mwaka 2015/2016, mamlaka hiyo ilisema kampuni ya Safaricom ilirekodi faida ya asilimia 66.3 ambayo imeshuka kwa kiwango cha asilimia 1.7 tangu mwaka uliotangulia.

Na hali ilikuwa hivyo hivyo kwa kampuni ya Airtel ambayo ndiyo mshindani wa karibu wa Safaricom. Kampuni hiyo nayo iliripoti kupungua kwa faida yake katika soko la hisa kwa asilimia 0.3, ambapo ilishuka hadi asilimia 19.1.

Kushuka huko kwa faida kumeripotiwa licha ya soko hilo la hisa kupata ongezeko la wateja wake kwa asilimia 4.7 na kufikia asilimia 37.8 kutoka asilimia 36.1, ambacho ndicho kiwango kilichoripotiwa mwaka jana.

Kulingana na ripoti hiyo kampuni hizo zimewapoteza wateja waliohama kufuatia kujibwaga uwanjani kwa wadau wapya kwenye nyanja hiyo ya mawasiliano kama vile makampuni ya Orange Kenya na Equitel ambayo inamilikiwa na benki ya Equity ambayo imeendelea kupata umaarufu nchini humo.

Mmoja wa wafanyakazi katika ofisi za makampuni ya mawasiliano
Mmoja wa wafanyakazi katika ofisi za makampuni ya mawasiliano

Kwingineko, kampuni ya Mobile Financial Services-MTN ya Uganda na ile ya Safaricom ya nchini Kenya zilitia saini makubaliano ya ushirikiano utakaowezesha wateja wao kubadilishana pesa kwa urahisi kupitia mitandao ya makampuni hayo.

Kwenye hafla ya kutiwa saini makubaliano hayo mkurugenzi wa fedha wa kampuni ya Safaricom, Betty Mwangi alisema kwamba ushirikiano huo ni dhahiri kwamba kampuni yake imepiga hatua kubwa katika mpango wake wa kuhakikisha kwamba wananchi wa nchi za Afrika mashariki wanafanya biashara bila pesa taslim hivi karibuni.

Mkataba huo mpya sasa umezileta pamoja nchi nne kufuatia ushirikiano na makampuni ya Safaricom ya Kenya, Vodacom ya Tanzania na MTN ya Rwanda.

Makubalkiano hayo kati ya Kenya na Uganda yatawawezesha watu zaidi ya milioni 26 ambao wamejisajili kama wateja wa Safaricom na MTN kupata huduma mbali mbali kupitia makampuni hayo.

XS
SM
MD
LG