Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 22:15

Polisi wa Ufaransa wamsaka mshambuliaji wa nane


Polisi wakisogelea gari iliyotia wasiwasi mjini Paris, Nov. 15, 2015.

PARIS - Polisi wa Ufaransa wametoa picha ya mtuhumiwa ambaye hajapatikana kutokana na mashambulizi ya Ijumaa usiku mjini Paris yaliyouwa watu wasiopungua 132.

Mtuhumiwa huyo ametambulishwa kama Salah Abdeslam mwenye umri wa miaka 26 na ambaye alizaliwa Belgium, Ublegiji. Tangazo la picha hiyo ya mtu anayedhaniwa kuwa mshamhuliaji wa nane humiwa inaonya kuwa ni mtu hatari na yeyote aliya na habari kuhusu yeye apige simu kwa polisi.

Ni mmoja kati ya ndugu watatu wanaohusishwa na mashambulizi ya Ijumaa mjini Paris.

Mmoja kati ya ndugu hao - Ibrahim Salah - alijilipua katika ukumbi wa muziki wa Bataclan katika shambulizi ambalo liliuwa zaidi ya watu 80. Maafisa wa Ubelgiji wanamshikilia ndugu wa tatu.

Polisi Ufaransa na Ubelgiji wamekamata watu kadha na wanahoji ndugu wa watu hao na watu wengine na wanaohusishwa na watuhumiwa wengine katika mashambulizi hayo.

XS
SM
MD
LG