Rais Barack Obama wa Marekani amelaani mashambulizi ya kigaidi ya Paris Ijumaa akisema "kitendo cha kuvuka mpaka kutishia watu wasio na hatia."
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari White House mjini Washington Rais Obama alisema Marekani iko tayari kutoa kila ushirikiano ambao Ufaransa inahitaji.
"Hili ni shambulizi dhidi ya ubinadamu na thamini zote tunazoshirikiana," alisema Rais Obama na kuongeza kuwa "Tuko tayari kutoa msaada wa aina yoyote ambao Ufaransa itahitaji."
Obama aliongeza kuwa " Hii ni hali ya kusikitisha, na bila shaka sisi hapa Marekani tunajua hii ina maana gani kwa sababu tumepitia matukio kama haya."
Obama alisema bado hajazungumza na Rais wa Ufaransa Francois Hollande, kutokana na mgogoro huo unaoendelea. Alikataa pia kusema serikali yake inatilia mashaka nani katika mashambulizi haya.
Ripoti zinasema kuwa watu wasiopungua 100 wameuawa katika matukio sita ya mashambulizi ya bunduki na mlipuko wa bomu mjini Paris mapema Ijumaa usiku.
CNN affiliate BFMTV reported at least 60 people were killed when six shootings and three explosions shook the French capital.