Baadhi ya wazazi wa wasichana wa shule 21 ambao walikuwa wametekwa nyara na wanamgambo nchini Nigeria Zaidi ya miaka miwili iliyopita, siku ya Jumatatu walikutana na wattoto wao.
Wasichana hao waliachiliwa huru siku ya Alhamisi na wakasafirishwa kwa ndege hadi Abuja, mji mkuu wa Nigeria, lakini ilichukua siku kadhaa kabla ya wazazi wao kuwasili kutoka vijijini mwao.
Hii ni mara ya kwanza kwa wasichana hao wa Chibok kuachiliwa huru kufuatia makubaliano yaliyoongozwa na shirika la msalaba mwekundu na serikali ya Uswizi.
Karibu wasichana 300 walitekwa kutoka kwenye shule yao mnamo mwaka wa 2014 katika mji wa chibok uliopo katika jimbo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, ambako kundi la Boko Haram limekuwa likipigana likitaka kuanzishwa kwa taifa la Kiislamu, na kuwaua maelfu ya watu na kuwaacha Zaidi ya milioni mbili bila makao.