Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 23:34

Wanasayansi wavumbua kifaa cha kutibu kupooza viungo


Majaribio yaliyofanywa kwa nyani yameonyesha kuwa huenda binadamu akafaidika na teknolojia hiyo.
Majaribio yaliyofanywa kwa nyani yameonyesha kuwa huenda binadamu akafaidika na teknolojia hiyo.

Wanasayansi wa Uswizi wamefanya majaribio yaliyofana wa kifaa ambacho huenda kitaweza kuwasaidia watu waliopoteza uwezo wa kutumia mikono na miguu yao, kuitumia tena.

Chombo hicho, kinachojulikana kama Neuroprosthetic interface, kilitengenezwa na timu ya kimataifa katika chuo cha serikali kilicho mjini Lausane, nchini Uswizi.

Gregorire Courtine, manasayansi aliyeuongoza mradi huo, anaseama chombo hicho kina uwezo wa kusoma ishara za kile ubongo inataka kufanya, na kutuma ujumbe kwa uti wa mgongo chini ya eneo la jeraha, na kuwezesha kiungo kilichoathirika kuweza kufanya kazi tena.

majaribio mawili kwenye nyani yaliwezesha mnyama huyo kutumia miguu yake iliyokua imepooza.

Chombo hicho kinatumia kidude cha kielektroniki ambacho kinadhibiti mguu na kutuma jumbe za kielektroniki kwa kompyuta , ambayo inasoma nia ya nyani kutumia mguu wake.

Gregoire anasema kuwa katika majaribio mawili yaliyofanywa, sehemu ya ubongo wa nyani na eneo husika la uti wa mgongo wa nyani hao, zilikuwa zinfanya kazi ipasavyo.

Chombo hicho kiliwezesha nyani hao kutumia tena miguu yao, jambo ambalo limewaqpa wanasayansi matumaini makubwa kwamba huenda kikafanya kazi kwa binadamu.

XS
SM
MD
LG