Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 09:09

Papa Francis ashutumu kuzorota kwa mzozo wa kibinadamu nchini Ethiopia

 Papa Francisco akiongoza sala ya malaika wa Bwana katika uwanja wa St.Peter Vatican.Januari 6,2021.
Papa Francisco akiongoza sala ya malaika wa Bwana katika uwanja wa St.Peter Vatican.Januari 6,2021.

Papa Francis siku ya Jumapili alishutumu kuzorota kwa mzozo wa kibinadamu nchini Ethiopia na kushinikiza mazungumzo ili kushinda vita hivyo vya muda mrefu.

Papa Francis siku ya Jumapili alishutumu kuzorota kwa mzozo wa kibinadamu nchini Ethiopia na kushinikiza mazungumzo ili kushinda vita hivyo vya muda mrefu.

Papa huyo katika mwonekano wake wa kila siku mbele ya umma katika uwanja wa St. Peter amesema alikuwa akifuatilia habari hiyo kwa wasiwasi kutoka Pembe ya Afrika, hasa kutoka Ethiopia, iliyotikiswa na mzozo ambao umedumu kwa zaidi ya mwaka mmoja na kusababisha waathiriwa wengi na janga kubwa la kibinadamu.

Vita katika eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia vimeua maelfu ya watu na kusababisha mamilioni wengine kuhama makazi yao na kuwaacha wengi wakihangaika na njaa kali.

"Ninaalika kila mtu kuwaombea wale watu waliojaribiwa kwa ukali sana, na ninasisitiza upya ombi langu ili maelewano ya kindugu na njia ya amani ya mazungumzo iweze kuwepo," Francis alisema.

XS
SM
MD
LG