Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 20:05

Papa Francis awataka vijana kuombea amani duniani


Pope Francis' apostolic journey to Portugal

Kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki Papa Francis alifunga tamasha la kimataifa la Vijana wa Kikatoliki siku ya Jumapili kwa kuongoza ibada kubwa, katika eneo lililo wazi, na hotuba yake aliyoiita "I have a dream", yani "Nina Ndoto," akisema inahusu amani ya dunia, hasa kwa Ukraine.

Takriban watu milioni 1.5 walihudhuria Misa hiyo katika bustani iliyo kando mwa mto katika mji mkuu wa Ureno, Vatikan ilisema, ikinukuu mamlaka za mitaa.

Wengi wa waumini walilala nje, wakihudhuria hafla ya mkesha wa tamasha hilo, Jumamosi usiku, na walikusanyika katika hali ya joto kali.

Akizungumza baada ya Ibada ya Misa Takatifu, Papa Francis mwenye umri wa miaka 86 aliwataka vijana kuupeleka undugu waliojifunza kwenye hafla hiyo ya siku sita nyumbani na kuutumia katika maisha yao ya kila siku.

"Wapenzi, niruhusu mimi, mzee, nishiriki nanyi vijana ndoto ambayo nimebeba ndani yangu: ni ndoto ya amani, ndoto ya vijana wanaombea hali ya amani, kuishi kwa amani na kujenga maisha ya baadaye yenye amani. " Francis alisema.

“Mnaporudi nyumbani tafadhali endeleeni kuombea amani, zaidi ya hayo ni ishara ya amani kwa dunia, mkionyesha jinsi mataifa, lugha na historia mbalimbali zinavyoweza kuungana badala ya kugawanyika, ninyi ni tumaini la ulimwengu tofauti. " alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG