Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 16, 2025 Local time: 19:26

Papa Francis atuma maombi yake ya kila Jumapili akiwa hospitalini


Picha ya hospitali ya Gemelli ambapo Papa Francis anaendelea kupokea matibabu mjini Rome. Machi 9, 2025 (Photo by ANDREAS SOLARO / AFP or licensor / AFP)
Picha ya hospitali ya Gemelli ambapo Papa Francis anaendelea kupokea matibabu mjini Rome. Machi 9, 2025 (Photo by ANDREAS SOLARO / AFP or licensor / AFP)

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis, ambaye afya yake imeendelea kuimarika wakati akipokea matibabu kutokana na homa ya mapafu, Jumapili aliwashukuru madaktari pamoja na wahudumu wa afya, ingawa hakuweza kuongoza maombi ya Angelus kwa mara ya nne mfululizo.

Papa Francis, mwenye umri wa miaka 88, na ambaye amelazwa kwenye hospitali ya Gemelli mjini Vatican tangu Februari 14, alituma maombi yake ya Angelus kwa njia ya maandishi akisema kwamba anashukuru wote ambao hujitolea kusaidia wengine wakati akisifu umoja wao pamoja moyo wa huruma. “Mimi mwenyewe hufikiria kuhusu utoaji wa huduma na huruma na hasa kutoka kwa madaktari na wahudumu wa afya, ambao nawashukuru kwa moyo wangu wote.”

“Tunahitaji “muujiza huo wa huruma” ili uandamane na watu wanaotaabika wakati ukiwapunguzia uchungu wanaopitia,” Papa alisema kupitia maandishi yaliyochapishwa na Vatican. Kiongozi huyo wa zaidi ya waumini bilioni 1.4 wa Kikatoloki kote duniani, aliwahi kulazwa kwenye hospitali hiyo ya Gemelli hapo awali wakati alipofanyiwa upasuaji wa utumbo 2021, pamoja na upasuaji wa hernia 2023.

Kulazwa kwa wakati huu hata hivyo kumekuwa na changamoto kadhaa wakati akishuhudia matatizo ya kupumua na kuzua wasi wasi kwamba hupona kwake huenda kukachukua muda mrefu, hali ambayo huenda ikapelekea kujiuzulu kwake.

Forum

XS
SM
MD
LG