Baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Liszt Ferenc mjini Budapest, Francis anatarajiwa kukutana na rais wa Hungary Katalin Novac na waziri mkuu wa Hungary Victor Orban na kisha kutoa hotuba yake kuu ya kisiasa kwa mamlaka na wanadiplomasia wa Hungary.
Anayo fursa ya kuzungumza na jumuiya ya Hungary na Ulaya kwa ujumla katika shughuli yake ya mwisho Jumapili wakati atakapo hutubia viongozi wa kitaaluma na kitamaduni katika chuo kikuu cha kikatoliki cha Budapest.
Maafisa wa Hungary wanasema safari ya Francis iliandaliwa kimsingi ili baba mtakatifu aweze kuhudumu katika nchi hiyo yenye jumuiya ya wakatoliki na kuwatia moyo waumini wake kiimani.
Lakini kutokana na vita vinavyoendelea karibu na Hungary ikipambana na mataifa mengine ya Umoja wa Ulaya kuhusu suala la utawala wa sheria na haki za LGBTQ, maneno ya Francis na matendo katika moyo wa Ulaya yatabeba msimamo mkali wa kisiasa.