Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 19:52

Papa Francis aonekana kuilenga China katika ziara Mongolia

Papa Francis akisalimiana na waumini nje ya Kanisa Kuu la Watakatifu Petro na Paulo huko Ulaanbaatar, Mongolia Jumamosi, Septemba 2, 2023. AP.

Francis mwenye umri wa miaka  86, alitoa maoni yake huko Mongolia, nchi ambayo ina Wakatoliki 1,450 pekee na ambapo Kanisa hilo ni  dogo nchini humo  na lina uhusiano mzuri na serikali ambayo imeonyesha kuthamini shughuli zake za kijamii, afya na hisani.

Papa Francis kwa maneno ambayo yalionekana kuilenga China badala ya nchi jirani aliyokuwa akiitembelea alisema Jumamosi kwamba serikali hazina chochote cha kuogopa kutoka katika Kanisa Katoliki kwa sababu halina ajenda ya kisiasa.

Francis mwenye umri wa miaka 86, alitoa maoni yake huko Mongolia, nchi ambayo ina Wakatoliki 1,450 pekee na ambapo Kanisa hilo ni dogo nchini humo na lina uhusiano mzuri na serikali ambayo imeonyesha kuthamini shughuli zake za kijamii, afya na hisani.

Katika siku yake ya kwanza nchini Mongolia, serikali ya nchi hiyo ilimpa heshima Papa kwa hafla za kitamaduni kwa gwaride likijumuisha wanaume waliopanda farasi waliovalia kama mashujaa wa zamani wa Mongolia.

Katika hotuba yake kwa maaskofu, mapadre, wamishionari na wachungaji alisema Yesu hakutoa mamlaka ya kisiasa kwa mitume wake bali aliwaambia wapunguze mateso ya binadamu waliojeruhiwa kwa imani.

Forum

XS
SM
MD
LG