Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 20:26

Papa Francis aomba radhi kuahirisha ziara yake DRC na Sudan Kusini


Papa Francis akiongoza sala ya Malaika wa Bwana kutoka dirishani kwake, Vatican, Juni 12, 2022.(Vatican media/Reuters).
Papa Francis akiongoza sala ya Malaika wa Bwana kutoka dirishani kwake, Vatican, Juni 12, 2022.(Vatican media/Reuters).

Papa Francis alisema Jumapili anatumai kuzuru Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan Kusini haraka iwezekanavyo, baada ya kuahirisha  ziara hiyo kutokana na tatizo la goti.

Papa Francis alisema leo Jumapili anatumai kuzuru Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan Kusini haraka iwezekanavyo, baada ya kuahirisha ziara hiyo kutokana na tatizo la goti.

"Wapendwa, kwa masikitiko makubwa, kutokana na matatizo ya mguu wangu, imenibidi kuahirisha ziara yangu katika nchi zenu," Papa huyo mwenye umri wa miaka 85 alisema baada ya sala yake ya kila wiki ya Angelus katika uwanja wa Mtakatifu Petro.

"Kwa kweli nina huzuni kubwa kwa kuahirisha safari hii, ambayo ina maana kubwa kwangu. Naomba radhi kwa hili.

Tuombe pamoja kwamba, kwa msaada wa Mungu na matibabu, niweze kuwa nanyi haraka iwezekanavyo. Wacha tuwe na matumaini!"

Vatican siku ya Ijumaa ilitangaza kuwa safari iliyopangwa kufanyika Julai 2 hadi 7 itaratibiwa upya, ingawa hakuna tarehe mpya iliyopangwa.

XS
SM
MD
LG