Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 14:04

Papa Francisi akemea maovu Mexico


Baba mtakatifu Francis amekemea uhalifu na kutokwa na usawa katika jamii wakati wa mahubiri na mazungumzo yake na viongozi wa kisiasa nchini Mexico.

Hapo Jumapili, kiongozi huyo wa kanisa Katoliki alifanya sala ya umma katika kitongoji cha eneo lenye uhalifu la Ecatepec.

Eneo hilo ni maarufu kwa ghasia dhidi ya wanawake.

Katika siku zilizosalia za ziara yake ya siku tano, Papa Francis pia atatembelea jamii ya watu masikini ya wa asili ya jimbo la Ciapas.

Vilevile Papa Francis atatembelea sehemu zinazo sumbuliwa na wafanyabiashara wa dawa za kulevya.

XS
SM
MD
LG