Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 16:32

Papa Benedicte XVI azuru Benin


Tangazo la ujio wa Papa Benedict XVI huko Benin.
Tangazo la ujio wa Papa Benedict XVI huko Benin.

Waumini na wafanyabiashara wajiandaa kumpokea Papa Benedicto XVI huko Benin.

Taifa dogo la Benin huko Afrika Magharibi linamkaribisha kiongozi wa Kanisa la Roman Katoliki Ijumaa huku waumini na wafanyibaishara wakikaribisha ziara hiyo kwa furaha. Wachuuzi wamekuwa wakiuza bidhaa za kidini kwa wiki kadha sasa katika barabara za mji mkuu Cotonou ambapo Papa Benedicte anatazamiwa kuanza ziara yake ya siku tatu nchini humo. Hii ni ziara ya pili kwa kiongozi huyo wa Kanisa la Roman Katoliki barani Afrika. Taifa la Benin lilikuwa mwenyeji wa Papa John Paul wa pili mwaka wa 1982 na 1993. Kuna maandalizi ya kila aina mjini humo pamoja na mikutano ya hadhara ya maombi. Waumini wa dini ya Roman Katoliki ndiyo wengi zaidi nchini Benin wakifuatiwa na Waislam. Lakini Benin haijawa na vurugu wala chuki za kidini kama inavyoshuhudia katika taifa jirani la Nigeria. Maafisa nchini humo wanabashiri kuwa ziara ya Papa Benedicte itakuwa njema na salama

XS
SM
MD
LG