Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 04:35

Papa awashukuru watu wa Sudan Kusini kwa upendo waliomuonyesha

Papa Francis, katikati, alipoongoza ibada ya Misa Takatifu kwenye Makaburi ya John Garang huko Juba, Sudan Kusini Jumapili, Februari 5, 2023.
Papa Francis, katikati, alipoongoza ibada ya Misa Takatifu kwenye Makaburi ya John Garang huko Juba, Sudan Kusini Jumapili, Februari 5, 2023.

Papa Francis aliwasihi  watu wa Sudan Kusini siku ya Jumapili kupinga “sumu ya chuki”  ili waweze kupata amani na ustawi ambao umewakimbia  kupitia miaka mingi ya vita vya kikabila vya  umwagaji damu.

Papa Francis aliwasihi watu wa Sudan Kusini siku ya Jumapili kupinga “sumu ya chuki” ili waweze kupata amani na ustawi ambao umewakimbia kupitia miaka mingi ya vita vya kikabila vya umwagaji damu.

Katika mazungumzo yake ya mwisho ya hadhara kabla ya kurudi nyumbani, Francis aliongoza Misa ya nje kwenye wwanja wa kaburi la shujaa wa ukombozi wa Sudan Kusini John Garang, aliyefariki mwaka 2005. Vatican ilisema watu 100,000 walihudhuria Misa hiyo.

Papa mwenye umri wa miaka 86 aliandaa mahubiri yake katika mada ambazo zimetawala safari yake katika taifa jipya zaidi duniani akilenga maridhiano na kusameheana kwa makosa yaliyopita. Aliwasihi waumini waepuke “ghadhabu ya upofu ya vurugu.”

Wengi katika umati huo waliimba, walipiga ngoma na vigelegele wakati Francis akiingia eneo hilo lenye vumbi, na mahubiri yake yalikatishwa mara kwa mara kwa kushangiliwa kwa nguvu na vigelegele zaidi.

Sudan Kusini yenye Wakiristo wengi ilijitenga na Sudan yenye waislam wengi mwaka 2011, lakini miaka miwili baadaye ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoua watu 400,000. Licha ya makubaliano ya amani ya 2018 kati ya wapinzani wakuu wawili, mapigano yaliendelea kusababisha vifo na kuwakosesha makazi raia wengi.

Mwishoni mwa ibada, katika hotuba ya kuaga muda mfupi kabla ya kuelekea uwanja wa ndege, Papa aliwashukuru watu wa Sudan Kusini kwa upendo waliomuonyesha.

XS
SM
MD
LG