Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 31, 2023 Local time: 15:59

Pande zote zinazohusika na mgogoro wa Ethiopia zadai ushindi


Wakimbizi wa Ethiopia wakusanyika mkoa wa Qadarif, mashariki Sudan, Jumapili, Novemba 15, 2020. Maelfu ya raia wa Ethiopia wanaokimbia vita mkoa wa Tigray kutafuta hifadhi Sudan (AP Photo/Marwan Ali)

Pande zote katika vita vinavyoendelea kaskazini mwa Ethiopia katika jimbo la Tigray zinadai ushindi wa kijeshi na kuzusha wasiwasi zaidi juu ya kuongezeka kwa mapigano licha ya kwamba serikali imedai utulivu na amani vitapatikana hivi karibuni. 

Kukatwa kwa mawasiliano katika jimbo hilo tangu Waziri Mkuu Abiy Ahmed kupeleka wanajeshi wake hapo Novemba 4 imekua vigumu kufahamu ukweli halisi wa mambo.

Hata hivyo Rais wa jimbo la Tigray, Debretsion Gebremichael akizungumza Alhamisi kwa mara ya kwanza tangu kuanza vita ameilaumu serikali ya Addis Ababa kwa kuomba msaada wa nchi za kigeni.

”Hao viongozi wawili wa kidikteta walipotambua kwamba ulinzi wetu ni mkali kuliko mashambulizi yao mnamo siku tatu zilizopita, wameomba msaada kutoka majeshi ya kigeni, huku ndege zisizo na rubani zikianza kutumiwa katika vita hivi,” amesema Gebremichael.

Kwa upande wake mkuu wa majeshi ya Ethiopia Berhanu Jula akizungumza na waandishi Alhamisi amemtuhumu mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani, WHO, Tedros Adhamon Ghebreyesus, ambae anatokea jimbo hilo la Tigray, kwa kutafuta silaha na ungaji mkono wa kigeni kuwasaidia viongozi wa Tigray.

Hivi sasa kutokana na wenzake ambao wanamawazo sawa, wanaungana pamoja, unatarajia nini kutoka kwake. Sisi hatukutajaria kamwe ataungana na watu wa Ethiopia ili kuwalaani hao wengine,” amesema Berhanu.

Vikiwa katika wiki yake ya tatu, vita vinazidi kuzusha wasiwasi katika jumuia ya kimataifa kukiwa na wito wa majadiliano kuanza.

Mshauri wa sera za mambo ya nje wa rais mteule wa Marekeni Joe Biden, kuhusu masuala ya kigeni Anthony Blinken ameomba raia wapatiwe ulinzi hasa wanaokimbia na kutaka usalama uimarishwe mara moja.

Blinken amesema “ Tuna wasiwasi mkubwa kuhusu mzozo wa kibinadamu nchini Ethiopia, ripoti za ghasia za kikabila, na hatari ya kuvurugika amani na usalama katika kanda hiyo”.

Tayari mzozo huo umesababisha vifo vya mamia ya watu na kulazimisha wengine elfu 30 kukimbila nchi jirani ya Sudan.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG