Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 00:18

Taarifa za siri za Panama zaikumba China


Delegates applaud as Chinese President, Xi Jinping, passes.
Delegates applaud as Chinese President, Xi Jinping, passes.

Nyaraka zilizotolewa kuhusu akaunti za benki na kampuni ya uwakili ya Panama zinaendelea kufichua taarifa kuhusu jamaa za viongozi wa chama cha kikomunisti cha China akiwemo rais wa nchi hiyo.

Kati ya stakabadhi milioni 11 zilizofichuliwa, kuna zile zinaelezea kuhusu akaunti za kigeni za jamaa za takriban viongozi 7 walioko serikalini pamoja na waliokuwa kwenye kamati ya bunge ya Politburo pamoja na kitukuu wa mwanzilishi wa chama cha Peoples Republic of China Mao Zedong.

Jumatano, jopa la waandishi wa habari wanaochunguza tukio hilo limesema miongoni mwa viongozi China wenye na akaunti za siri ni Deng Jiagui ambae ni shemeji wa Rais Xi Jingpin pamoja na Zeng Qinguai ambae ni ndugu wa aliekuwa Rais wa china Zeng Quighong.

XS
SM
MD
LG