Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 13:04

Pakistan yaaswa kupiga kura kutathmini mwelekeo wa Afghanistan


German Chancellor Angela Merkel

Maafisa wa Marekani na Afghanistan wametoa mwito kwa Pakistan kuhudhuria mkutano huo ambao una lengo la kuendeleza mkakati wa kuimarisha nchi jirani ya Afghanistan

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema anatarajia Pakistan itabadilisha mtazamo wake kuhusu kugomea kupiga kura katika mkutano wa kimataifa unaotarajiwa kufanyika kuhusu mwelekeo wa baadae wa Afghanistan.

Bi. Merkel alisema jumanne Serikali yake itajaribu kuwashawishi maafisa wa pakistan kubadilisha uamuzi wao kupinga majeshi ya NATO yaliyouwa wanajeshi 24 wa Pakistan wiki iliyopita katika mpaka wa Pakistan na Afghanistan.

Uamuzi wa Pakistan kugomea mkutano wa wiki ijayo ulitangazwa mapema leo.

Maafisa wa Marekani na Afghanistan wametoa mwito kwa Pakistan kuhudhuria mkutano huo ambao una lengo la kuendeleza mkakati wa kuimarisha nchi jirani ya Afghanistan kama majeshi ya pamoja yataondoka katika miaka ijayo.

Kiongozi mwandamizi wa jeshi la Marekani alisema jana Pakistan inatafuta sababu ya kuwa na hasira na mashambulizi ya anga ya NATO yaliyopiga katika maeneo kadhaa ya mpaka wa Pakistan jumamosi.


XS
SM
MD
LG