Taarifa hiyo imetolewa saa chache baada ya IMF kutangaza makubaliano ya mwanzo na Islamanad kutoa mkopo wa dola bilioni 7 wa muda wa miezi 37.
Mkopo huo unasubiri kuidhinishwa na bodi ya utendaji ya IMF na kujpatikana kwa mkopo huo ni muhimu kwa Pakistan kwa ajili ya mipango yake ya maendeleo.
Hakuna tarehe kamili ambayo bodi ya IMF itaidhinisha mkopo huo, lakini ni hatua ya mchakato tu kabla ya pesa kutolewa.
Waziri mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif ametangaza taarifa hiyo leo Jumamosi wakati wa kikao na timu yake ya wataalam wa fedha na kuwasifu kwa kufanya mazungumzo yaliyopelekea kupatikana kwa mkopo huo.
Forum