Mamlaka nchini Pakistan leo Alhamis zimemuachia huru kutoka gerezani mke wa waziri mkuu wa zamani Imran Khan, ikiwa ni miezi tisa baada ya wawili hao kuhukumiwa kwa tuhuma za ufisadi.
Mke wa waziri mkuuu wa zamani Bushra Bibi aliruhusiwa kuondoka katika gereza la Adiala lililopo karibu na Islamabad, siku moja baada ya mahakama kuu ya serikali kuidhinisha ombi lake la dhamana. Viongozi wa chama cha Khan, cha Pakistan Tehreek-e-Insaf au PTI wamesema Bibi alisafiri hadi kwenye makazi yake nje kidogo ya mji mkuu wa Pakistan baada ya kuachiliwa huru.
PTI iliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa X, “karibu Bibi”. Khan mwenye miaka 72, na Bibi walihukumiwa kifungo cha miaka 14 mwezi Januari kwa tuhuma za kuhifadhi na kuuza zawadi za serikali kinyume cha sheria alizopokea wakati wa uongozi wake kuanzia mwaka 2018 hadi 2022.
Baadaye walipatikana na hatia na kupewa hukumu ya ziada katika kesi nyingine kadhaa, ikijumuisha mashtaka ya ndoa haramu.
Forum