Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 05, 2022 Local time: 03:21

Pakistan na China kushirikiana kibishiara


Meli ya mizigo kwenye bandari ya Gwadar Pakistan

Pakistan na China wiki hii zimezindua njia mpya ya bishara ya kimataifa kupitia bandari ya kusini magharibi mwa Pakistan ya Gwadar.

Pakistan na China wiki hii zimezindua njia mpya ya bishara ya kimataifa kupitia bandari ya kusini magharibi mwa Pakistan ya Gwadar ikiwa njia moja ya kuonyesha ushirikiano wa kiuchumi wenye dhamani ya mabilioni ya dola baina ya mataifa hayo mawili.

Uwekezaji wa China wa dola bilioni 46 chini ya mpango wa njia ya kiuchumi kati ya China na Pakistan utapelekea kujengwa kwa barabara, njia ya reli na njia ya mawasiliano pamoja na miradi ya kutoa nishati kati ya eneo la magharibi mwa China la Xinjiang na Gwadar nchini Pakistan.

Mradi huo utafungua bandari ya Gwadar iliotengenezwa na fedha pamoja na ufundi kutoka China kuwa kiingilio cha kuagizia na kusafirisha bidhaa kutoka jimbo la magharibi la china la Xinjiang kuelekea kwenye soko la kimataifa.

XS
SM
MD
LG