Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 12:48

Ouattara atoa wito kumalizika ghasia za wahamiaji Ivory Coast


Rais anayetambulika kimataifa nchini Ivory Coast, Alassane Ouattara(R) akiwa na mwenyekiti wa tume ya AU, Jean Ping(L) huko Abidjan, Ivory Coast.
Rais anayetambulika kimataifa nchini Ivory Coast, Alassane Ouattara(R) akiwa na mwenyekiti wa tume ya AU, Jean Ping(L) huko Abidjan, Ivory Coast.

Kiongozi anayetambulika kimataifa kama mshindi wa uchaguzi wa kiti cha Rais nchini Ivory Coast, ameatoa wito wa kumalizika ghasia dhidi ya wahamiaji.

Alassane Ouattara alisema Jumanne kwamba wahamiaji wanakaribishwa kukaa Ivory Coast. Alisihi kila mmoja kusaidia kujenga nchi yenye ukarimu ambao unakwenda zaidi ya ushirika wa damu. Bwana Ouattara alizungumza kutoka kwenye hoteli moja huko Abidjan, ambapo analindwa na vikosi vya Umoja wa Mataifa.

Kundi la Human Rights Watch, linayashutumu majeshi yanayomtii Rais Laurent Gbagbo anayeng’ang’ania madaraka kwa kuwalenga wahamiaji kutoka Mali, Burkina Faso, Nigeria na Niger, kwa kuwapiga na hata kuwachomea nyumba zao.

Kundi hilo pia lilisema ghasia zilizofanywa na majeshi yanayomuunga mkono Gbagbo katika miezi mitatu iliyopita, ikiwemo ubakaji na mauaji huenda zikawa uhalifu wa vita. Mapigano yanaendelea huko Abidjan na katika eneo la magharibi ya nchi. Mashahidi wanaripoti mapigano makali katika mji wa Duekoue, karibu na mpaka na Liberia.

Waasi wa kundi la New Forces ambao wanamuunga mkono bwana Ouattara wameingia kusini katika eneo lililoshikiliwa na majeshi ya mpinzani wake. Kundi hilo la uasi linasema limeteka miji minne katika eneo la magharibi kutoka kwa majeshi yanayomuunga mkono Gbagbo katika wiki za hivi karibuni.

XS
SM
MD
LG