Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 21:52

Ouattara awataka raia kutulia Ivory Coast


Majeshi yanayomuunga mkono Alassane Outtara.
Majeshi yanayomuunga mkono Alassane Outtara.

Katika hotuba iliyotolewa kwenye televisheni Alhamisi Bw. Ouattara aliliambia taifa hilo kuwa majeshi yake yameweka vizuizi kwenye jumba la rais.

Rais anayetambulika kimataifa wa Ivory Coast Alassane Ouattara amewataka raia wote wa Ivory Coast kujiepusha na vitendo vya ghasia wakati wa juhudi zikiendelea kurejesha ushwari nchini humo.

Katika hotuba iliyotolewa kwenye televisheni Alhamisi Bw. Ouattara aliliambia taifa hilo kuwa majeshi yake yameweka vizuizi kwenye jumba la rais mjini Abidjan ambako mpinzani wake Laurent Gbagbo alizuiwa. Bw. Gbagbo anadai alishinda uchaguzi wa Novemba na amekataa kuachia madaraka.

Bw. Ouattara amesema mpinzani wake amekataa kuachia madaraka na ameiingiza nchi kwenye mzozo wa kibinadamu. Lakini amesema uhalifu uliofanyika wakati wa mapigano hayo utafanyiwa uchunguzi na wahusika kuadhibiwa.

XS
SM
MD
LG