Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 26, 2024 Local time: 11:00

Ouattara amfukuza kazi mkuu wa baraza la katiba


Rais Alassane Ouattara.
Rais Alassane Ouattara.

Rais wa Ivory Coast amemfuta kazi mkuu wa baraza la katiba nchini humo, mtu ambaye alimuunga mkono rais wa zamani Laurent Gbagbo wakati wa mzozo wa karibuni wa kisiasa nchini Ivory Coast.

Nafasi ya Paul Yao N'dre imechukuliwa na mwanasiasa mkongwe Francis Wodie, mgombea wa zamani wa urais. Rais Alassane Ouattara alimteua Wodie katika agizo maalum.

N'dre alisaidia kuchochea mapambano ya madaraka kati ya Bwana Ouattara na Bwana Gbagbo ambayo yalifuata baada ya uchaguzi wa rais wa mwezi Novemba.

Tume ya uchaguzi ya Ivory Coast ilimtaja Bwana Ouattara mshindi, lakini N'dre alitumia mamlaka yake kama mkuu wa baraza la katiba, kutupilia mbali kura takriban nusu milioni za Ouattara kutoka kwenye ngome zake na kumpa ushindi Bwana Gbagbo.

N'dre baadae alibadili uamuzi wake baada ya waasi wanaomuunga mkono Ouattara kukamata udhibiti wa nchi na kumkamata Bwana Gbagbo mjini Abidjan.

Alimuapisha Bwana Ouattara kama rais wa Ivory Coast mwezi Mei.

Umoja wa Mataifa inasema miezi minne ya mapambano ya madaraka kati ya wafuasi wa Ouattara na Gbabo yamesababisha vifo vya takriban watu 3,000 na kuwakosesha makazi zaidi ya milioni moja.

XS
SM
MD
LG