Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 17:03

Kanali wa Jeshi Korea Kaskazini akimbilia Kusini


Wanajeshi wa Korea Kaskazini wakiwa katika gwaride mjini Pyongyang.
Wanajeshi wa Korea Kaskazini wakiwa katika gwaride mjini Pyongyang.

Korea Kusini inasema ofisa mmoja wa jeshi mwenye cheo cha juu huko Korea Kaskazini ameasi kuelekea kusini mwaka jana.

Tangazo hilo limetangazwa leo Jumatatu na wizara za ulinzi na ushirikiano wa pamoja za kusini, hali ambayo inatokea karibu na kukamilika kwa masuala ya ndani kati ya mahasimu hao wa Korea.

Ofisa huyo ni kanali ambaye alifanya kazi kama jenerali katika idara ya upelelezi kaskazini, na kumfanya awe ofisa wa cheo cha juu kabisa kuwahi kuasi kutoka utawala huo.

Kitengo hicho kinahusika na harakati za upelelezi dhidi ya Seoul ikiwemo mashambulizi ya mtandao. Kitengo hicho pia kinalaumu shambulizi la kuzamisha meli la mwaka 2010 dhidi ya meli ya Korea Kusini, ambayo iliuwa mabaharia 46, kitendo ambacho Pyongyang inakanusha.

XS
SM
MD
LG