Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 05:24

Oscar Pistorius kutoka gerezani


Oscar Pistorius aliposhiriki mashindano ya riadha katika michezo ya walemavu iliyofanyika London mwaka 2012. Picha na IAN KINGTON / AFP.

Raia wa Afrika Kusini bingwa wa Olimpiki ambaye ni mlemavu Oscar Pistorius huenda akaachiliwa kutoka jela wiki hii, ni muongo mmoja tangu apatikane na hatia ya kumuua mpenzi wake katika uhalifu uliuoigusa ulimwengu.

Bodi ya msamaha itatoa uamuzi endapo Pistorius ataachiwa mapema, baada ya kesi hiyo kusikilizwa mjini Pretoria siku ya Ijumaa.

"Bodi lazima iamue iwapo lengo la kifungo cha jela limetekelezwa," msemaji wa Idara ya Huduma za Magereza Singabakho Nxumalo alisema.

Pistorius, ambaye sasa ana umri wa miaka 36, alihukumiwa kwa kosa la kumpiga risasi na kumuua mwanamitindo Reeva Steenkamp, alfajiri ya Siku ya Wapendanao mwaka 2013, Pistorius alipofyatua risasi mara nne kupitia mlango wa bafuni ndani ya nyumba yake ambayo ilikuwa katika eneo lenye ulinzi mkali mjini Pretoria.
Alikana shitaka hilo, na kwa hasira alikataa kuhusika na mauaji ya Steenkamp, akisema alifyatua risasi alimdhania kuwa mwizi.

Mwanamichezo huyo anajulikana duniani kote kama "Blade Runner" kwa sababu ya kutumia viungo bandia, alihukumiwa kifungo cha miaka 13 jela.

Tangu ahukumiwe 2014, Pistorius ametumikia zaidi ya nusu ya kifungo hicho.

Wahalifu nchini Afrika Kusini moja kwa moja wanastahiki kupewa msamaha baada ya kutumikia nusu ya vifungo vyao.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG