Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 03:56

Orodha ya majina mapya juu ya shambulizi la sept 11 yajitokeza


Jengo la World Trade Center lililoshambuliwa na magaidi September 11, 2001.
Jengo la World Trade Center lililoshambuliwa na magaidi September 11, 2001.

Orodha ya majina mapya ambayo yanauwezekano kuhusishwa na Saudi Arabia kwenye mashambulizi ya ugaidi ya Septemba 11, 2001 mjini New York na Washington imejitokeza wakati ambapo Rais Barack Obama anafikiria iwapo atoe ripoti ya siri ya kurasa 28 kuhusu uhusiano unaoshukiwa wa Riyadh kusaidia msaada wa fedha za mashambulizi ambayo yaliuwa takribani watu 3,000.

Nakala zinazojulikana kama File 17 zinaorodhesha zaidi ya majina ya watu 30 wengi wao raia wa Saudi Arabia ambao walikutana au walizungumza na baadhi ya watekaji ndege ambao waliteka ndege za abiria na kuzigonga kwenye majengo ya kituo cha biashara duniani-World Trade Center mjini new York na Pentagon mjini Washington. Watekaji ndege 15 kati ya 19 walikuwa raia wa Saudi Arabia.

Seneta wa zamani wa Florida, Bob Graham.
Seneta wa zamani wa Florida, Bob Graham.

Seneta wa zamani wa Marekani, Bob Graham wa jimbo la Florida ambaye pia alikuwa mwenyekiti mwenza wa tume inayochunguza shambulizi la Septemba 11 aliliambia shirika la habari la Associated Press kwamba taarifa nyingi katika nakala ya File 17 ilitokana na ripoti ya kurasa 28 ambayo Obama anaifikiria sio siri tena.

Graham anaamini watekaji ndege walikuwa na mfumo wenye msaada thabiti wa Saudi Arabia ndani ya Marekani kabla ya kufanya mashambulizi akisema kwamba vipengele vya kurasa 28 za siri za ripoti ndefu juu ya mashambulizi vinaelekeza “namna Saudi Arabia ilivyokuwa mtoaji fedha mkuu”.

File 17 ilisema haya ni baadhi ya maswali ya ziada yasiyopata majibu na hivi ndivyo tunavyofikiria tume inayofuatilia mashambulizi ya Septemba 11, FBI na CIA wanatakiwa kufanya utafiti wa kupata majibu haya alisema Graham.

Ramani ya Saudi Arabia ikionesha miji ya Riyadh, Jeddah na mingineyo
Ramani ya Saudi Arabia ikionesha miji ya Riyadh, Jeddah na mingineyo

File 17 kwanza ilitolewa na mtandao wa 28pages.org kundi moja la wanaharakati linalotoa wito wa kutolewa kwa nakala za siri, orodha ya mawasiliano ambayo wa-Saudia walikuwa nayo na watekaji ndege wengi wao kutoka magharibi mwa jimbo la California nchini Marekani. Taarifa nyingi kwa jumla zimekuwa zikijulikana kwa miaka kadhaa lakini suala ambalo gumu kuelezea ni uwezekano wa Saudi Arabia kuhusika katika mashambulizi ya Septemba 11 linabaki kuwa maslahi muhimu katika Marekani.

Saudi Arabia imekuwa ikirudia kusema kwamba shutuma hizi hazina ukweli wowote. Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia, Adel al-Jubeir aliwaambia waandishi wa habari mjini Washington kwamba hakuna ukweli juu ya suala hilo.

XS
SM
MD
LG