Vyama vya upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, vimetishia kuitisha maandamano tarehe 24 mwezi huu kishinikiza Tume huru ya uchaguzi kutoa kalenda ya uchaguzi.
Hata hivyo serikali imepanga mikakati ya kufanyika kwa mazungumzo baina yake na vyama hivyo swala ambalo viongozi wa upinzani wanasema ni la kuwapotezea muda tu.