Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 07, 2022 Local time: 03:41

Upinzani DRC waongoza viti vya bunge


Wafanyakazi wa tume ya uchaguzi nchini DRC wakihesabu kura katika kituo kimoja cha uchaguzi nchini humo

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa bunge DRC yanaonesha upinzani umejizolea viti vingi

Wabunge wa upinzani nchini DRC wamechukua viti vingi vya chama cha Rais kabila katika bunge, ingawa bado chama hicho kinaongoza katika bunge hilo.

Matokeo ya awali yaliyotolewa Ijumaa na tume huru ya uchaguzi ya nchi hiyo –CEN yameonesha chama cha Rais kabila cha PPRD kimeshinda viti 58 – vingi kuliko vyama vingine katika uchaguzi wa bunge nchini Drc.

Lakini matokeo hayo yanakiweka chama cha PPRD katika mwelekeo wa kushinda viti vichache kuliko vile 111 ilivyoshinda mwaka 2006 ikimaanisha kuwa PPRD itahitaji uungwaji mkono kutoka vyama vingine washirika ili kupata wingi katika viti 500 vya bunge.

Chama cha kiongozi wa upinzani Etiene Tshisekedi cha UDPS kilishika nafasi ya pili kwa kupata viti 34. Tume huru ya uchaguzi pia imetoa wito kwa matokeo kubatilishwa katika wilaya saba ambako mapigano yaliharibu upigaji kura.

Maafisa wa uchaguzi walisema wagombea kadhaa walioshutumiwa kuchochea ghasia wapelekwe kwenye vyombo vya sheria.

Upigaji kura wa viti vya wabunge ulifanyika Novemba 28, siku moja na uchaguzi wa Rais.Wakati bwana Kabila alipotangazwa mshindi, bwana Tshisekedi aliyapinga matokeo na alijaribu kujiapisha mwenyewe kama Rais wa nchi hiyo, mwezi mmoja baadae.

Wafuatiliaji wa kimataifa pia waliukosoa upigaji kura huo ambao uligubikwa na ghasia pamoja na wizi wa kura.

XS
SM
MD
LG