Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 07:35

Zoezi la uokozi wa wahamiaji laendelea katika pwani ya ugiriki


mhamiaji akisubiri chakula kaskazini mwa ugiriki.
mhamiaji akisubiri chakula kaskazini mwa ugiriki.

Miili ya watu wanne imegunduliwa na wahamiaji wengine 342 kuokolewa kufuatia operesheni ya uokozi wa wahamiaji, waliokuwa kwenye boti lilokumbwa na ajali na kupinduka katika bahari ya Mediterranean mapema Ijumaa. Hayo ni kwa mujibu wa maafisa wa Ugiriki.

Zaidi ya watu 700 inaaminika walikuwa katika boti hiyo ilipoanza kuzama mapema Ijumaa.

Msemaji wa walinda usalama katika pwani ya Ugiriki alisema kwamba waokoaji walikuwa wameingia baharini na kutupa mipira ya uokozi na wanaendelea kuwaokoa wahamiaji hao. Alisema idadi ya watu walioathiriwa inakisiwa kuwa ni mamia.

Haikujulikana mara moja boti hilo lilikuwa limetokea wapi wala uraia wa abiria wake. Raia wa Nigeria na Gambia ni baadhi ya wahamiaji wanaofanya safari kutoka Libya kuelekea Ugiriki, hata ingawa idadi ya Wasomali na Waeritrea wanaotoroka makwao pia imeongezeka.

XS
SM
MD
LG