Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 14, 2024 Local time: 23:04

Ongwen afikishwa mahakamani The Hague


Jeshi la Uganda People's Defence Force-UPDF likimkabidhi Dominic Ongwen, mwenye shati la buluu kwa kikosi cha Umoja wa Afrika
Jeshi la Uganda People's Defence Force-UPDF likimkabidhi Dominic Ongwen, mwenye shati la buluu kwa kikosi cha Umoja wa Afrika

Kiongozi wa juu wa kundi la waasi la Lord’s Resistance Army-LRA amefikishwa kwa mara ya kwanza kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu huko The Hague na kuhitimisha msako wa muda mrefu ya kumfikisha mbele ya sheria. Mtuhumiwa huyo ni kamanda wa uasi Dominic Ongwen anayekabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Dominic Ongwen alikuwa akitafutwa kwa zaidi ya muongo mmoja na mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC. Jumatatu alisimama mbele ya mahakama hiyo huko The Hague kwa mara ya kwanza.

Akiwa amevaa suti ya buluu iliyokoza na tai, Ongwen alijitambulisha kwa mahakama hiyo kwa lugha ya Acholi ambayo inazungumzwa na wengi katika eneo analotokea la kaskazini mwa Uganda. Alisema alitekwa mwaka 1988 na kuchukuliwa msituni akiwa na umri wa miaka 14. Alisema alikuwa mwanajeshi wa LRA.Pia alimshukuru mungu kwa kuweka pepo, ardhi na watu wake.

Dominic Ongwen
Dominic Ongwen

Baada ya kujisalimisha mwenyewe mwezi uliopita huko Jamhuri ya Afrika ya kati-CAR, Ongwen alikamatwa na kupelekwa The Hague. Anakabiliwa na mashtaka dhidi ya uhalifu wa binadamu na uhalifu wa vita ambayo ni pamoja na mauaji, kuwatumikisha watu, vitendo visivyo vya kibinadamu na kuongoza mashambulizi dhidi ya raia. Yote hayo yanaelezewa ni katika shambulizi la mwaka 2004 kwenye kambi ya watu wasiokuwa na makazi kaskazini mwa Uganda.

Yeye ni miongoni mwa wanachama wa juu wa kundi la LRA wanaotafutwa na mahakama ya The Hague.

Hivi sasa Ongwen akiwa na umri wa miaka 34 alipandishwa vyeo kutoka mwanajeshi mtoto. Mawakili wake wanatarajiwa kutumia matatizo aliyokabiliana nayo siku za nyuma kama hoja ya kuomba ahurumiwe.

XS
SM
MD
LG