Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 14:14

Mateen alisema aliua watu kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya Syria na Iraq


Ronald Hopper wa FBI akizungumza na waandishi wa habari.
Ronald Hopper wa FBI akizungumza na waandishi wa habari.

Mshambuliaji aliyeuwa watu huko Orlando Omar Mateen awali alizungumza kwa lugha ya kiarabu na kujitangaza kuwa ni askari wa kiislam wakati wa mazungumzo ya simu na wafanyakazi wa dharura wakati akiuwa watu 49 katika mauaji mabaya kuwahi kutokea katika historia ya Marekani kwa mujibu wa FBI.

“Niko Orlando na nimepiga watu risasi” mshambuliaji huyo alimwambia opareta wa simu ya dharura 911 katika simu yake ya kwanza kutoka klabu ya Pulse alfajiri ya Juni 12 kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatatu.

Taarifa hiyo imetoa mambo mapya machache juu ya mashambulizi hayo.

Nyaraka hizo zilifanyiwa marekebisho kwa kiasi kikubwa kuondoa kile maafisa wanachosema kuwa ni tangazo la Mateen la kuunga mkono kundi la ISIS na kiongozi wake Abu bakr al Baghdadi. Maafisa pia wamekataa kutoa sauti ya mazungumzo hayo.

Spika wa bunge Paul Ryan, siku ya Jumatatu alipinga kutolewa kwa taarifa iliyohaririwa.

Mshambuliaji huyo wa Orlando ambaye baadaye aliuwawa na Polisi pia alifanya mazungumzo mengine ya simu na wasuluhishi na kusema alifanya hayo kutokana na mashambulizi ya Marekani huko Syria na Iraq.

XS
SM
MD
LG